Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, gazeti la Wall Street Journal limeripoti likinukuu vyanzo vyenye habari kuwa mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner, mkwe wa rais Donald Trump, wameandaa mpango wa kuingilia kati masuala ya Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jambo pekee lililo wazi katika mradi huo wa miaka 10 ni gharama ya dola bilioni 112, na haijulikani jinsi Wapalestina milioni 2 wanaoishi Gaza watakavyohifadhiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi.
Afisa mmoja wa Marekani ameliambia Wall Street Journal kwamba maelezo ya mradi huo yameshawasilishwa kwa "nchi zinazoweza kutoa ufadhili, zikiwemo nchi tajiri za Ghuba, Uturuki na Misri".
Wall Street Journal iliandika kuwa mpango huo uliandaliwa na wasaidizi wa White House kwa kushauriana na maafisa wa Israel. Hata hivyo, baadhi ya maafisa wa Marekani wana shaka kubwa juu ya uwezekano wa kutekelezwa kwa mpango huo kutokana na changamoto kama vile upokojaji silaha wa Hamas.
Your Comment